WASIFU WA MTOA MADA
Kwa ufupi kuhusu Dkt. Amina Msengwa
Dkt. Amina Msengwa
Mtakwimu Mkuu wa Serikali
Ni Mtakwimu Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiongoza juhudi za taifa letu katika kutoa takwimu rasmi zenye ubora wa hali ya juu, kwa wakati na zinazotegemewa ili kusaidia maamuzi yanayozingatia ushahidi wa kitakwimu na maendeleo ya kitaifa.
Dkt. Amina Msengwa amekuwa Mtakwimu Bingwa Mbobezi katika masuala ya Monitoring and Evaluation, na Mhadhili mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa zaidi ya miaka 22.
