WASIFU WA MTOA MADA

Kwa ufupi kuhusu Dkt. Victor Eliah

Speaker 1

Dkt. Victor Eliah

Mtayarishaji wa Vipindi Mwandamizi TBC

Dkt. Victor Eliah ni Mtozi (Mtayarishaji wa vipindi vya Televisheni) Mwandamizi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Ana shahada ya Uzamivu (PhD) ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma - Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ana shahada ya Uzamili (Masters) ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Elimu na Televisheni, Ana shahada ya Elimu (Katika Kiswahili, Redio na Televisheni) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Ana Cheti cha Utayarishaji wa Makala fupi na uhariri wa vipindi vya Televisheni kutoka Canal France International (CFI) aliyopata Kenya,na Cheti cha Utayarishaji na Usambazaji wa Maudhui ya Televisheni katika ngazi ya Kimataifa yaani Global Broadcasting Content Production and Distribution kutoka RAPA – nchini Korea Kusini, Ana tuzo mbalimbali za Umahiri zikiwamo ya Uandishi wa Habari za Utalii ya MCT mwaka 2016 na utayarishaji bora wa vipindi vya Lugha ya Kiswahili Tanzania kutoka Serikalini - Mwaka 2022, Ni mwandishi wa Vitabu 5, viwili vya Television Production na 3 vya Kiswahili katika vyombo vya Habari

Ni Mwandishi wa Makala(Articles) katika Journals za Kimatifa mfano Predictors of Television Programmes Quality in Tanzania: Analysis of Stakeholders’ Perspectives: ya Mwaka 2021: Imechapishwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (University of Dar es Salaam Library Journal), Analysing Television Captioning: Production, Readings and Effects (2024) Imechapishwa na Jarida la Asian Research Journal of Arts & Social Sciences: India. Pia ni Peer Reviewer Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Kiswahili la Taifa - BAKITA), Ni Meneja wa Televisheni TBC. Pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tanzania Safari Channel.

KIKAO KAZI CHA MAAFISA HABARI WA SERIKALI, 2025